Wednesday, February 20, 2013

SHAMBULIO LILILOWAADHIRI WATALII WA KITALIAONO KTK VISWA VYA MALINDI KENYA.


somalimemo.netWatu waliojihami na silaha wamefanya shambulio ktk Mji wa Malindi Pwani mwa Kenya eneo la watalii wazungu na kuna hasara lililosababisha shambulio hilo.
Chanzo cha habari zinaeleza kuwa mtu alieficha uso alifanya shambulio ktk eneo wanaopenda watalii wa Kizungu kutoka Italia.
Maofisa wa Uslama wanasema mtu aliyejihami na silaha nzito aliwafyatulia risasi watalii waliokuwa wakipumzika eneo la ufukwe mwa bahari.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema baada ya tukio hilo kufanyika watu walikimbilia kwenda kushudia ktk eneo la tukio na huenda mashambulio yakaongezeka kwani watalii baado wako ktk eneo hilo.
Watu waliojeruhiwa walikimbizwa ktk Hospitali ya Kenyatta Mjini Nairobi na kufanyiwa matibabu zaidi,Wengi waliojeruhiwa ni watalii wazungu kutoka Nchini Itali na Baadhi ya Nchi za Magharibi ziliwaonya Wananchi wake kutembelea Nchi ya Kenya kutokana na Usalama wa Nchi hiyo kutoweka ktk miezi zilizopita.
Uchaguzi unaotarijiwa kufanyika hivi karibuni nchini Kenya unahofiwa kutokea mashambulio zaidi kutokana na Makundi yanayofanya Mashambulio Nchini kenya kuwa na nguvu zaidi Ktk Miji Mikubwa Nchini Kenya,baada ya Nchi hiyo kujiingiza Kijeshi ktk Ardhi ya Kislaam ya Somalia

No comments:

Post a Comment