Da'wa


 QUR-AN.
 Qur-an ni ujumbe sahihi kutoka kwa Allah (s.w) wenye lengo
la kumuongoza binaadamu katika njia sahihi ya maisha itakayo
muwezesha kuishi kwa furaha na amani hapa duniani na kuwa na
makazi mema na furaha ya milele huko akhera. Katika kuongoza
kwake, Qur-an humuwezesha binaadamu kujitambua kuwa yeye ni
nani na kumfahamisha lengo la maisha yake hapa duniani na
namna ya kulifikia. Pia Qur-an inamuweka wazi binaadamu kuwa
ataishi hapa duniani maisha ya dhiki yenye kuzingirwa na hofu na
huzuni na katika maisha ya akhera atakuwa na dhiki kubwa zaidi
na huzuni ya kudumu endapo ataikhalifu Qur-an kama
tunavyokumbushwa katika aya zifuatazo:


“Na atakayejiepusha na mawaidha yangu (Qur-an), basi
kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na siku ya kiyama
tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: “Ee Mola wangu!

Mbona umenifufua kipofu, hali nilikuwa nikiona?” (Allah)
atasema, “Ndiyo vivyo hivyo. Zilikujia aya zetu ukazisahau
(ukazipuuza) na kadhalika leo utasahauliwa (utapuuzwa).Na
h i v i n d i v y o t u t a k a v y oml i p a k i l a a p i t a y e k i a s i
(anayepundukia mipaka) na asiyeamini aya za Mola wake,
na bila shaka adhabu ya akhera ni kali zaidi na iendeleayo
sana.” (20:124-127).


UNAWEZA KUPATA TAFSIRI YA QURAN ZIFUATAZO:
JALALAIN

TARJUMA YA KISWAHIL

tafsiri ya ibn abbas

"Tawassul" Ni neno lenye kusikika Sana hasa siku hizi ambapo kumejitokeza baadhi ya walimu humu mwetu kutetea Tawassul zisizofaa kisheria kwa sababu tu walimu hao wamezifanya ndio kitega uchumi kikubwa katika maisha yao. Hivyo pale walipojitokeza vijana watetezi wa Dini na sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)(ANSWAAR) kuhadharisha ndugu zao Waislam na utapeli unaofanywa na walimu hao kwa jina la dini basi walimu hao wamekua wakali sana kutetea ‘ulua’ huo, na kutumia Aya na Hadithi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)kuzifasiri wanavyotaka wao au kutumia Hadithi za Uongo ilimradi tu "ulua" wao uendelee.
Kwa sababu Waislamu wengi waliingia katika mtego huu ilikua mtu hawezi kuanzisha biashara, kuhamia nyumba mpya au kununua gari mpaka amwite mwalimu amsomee ‘Tawassul’ ima ya ‘Nabahan’ au ‘Ahalalbadri’ au nyinginezo bila ya kujua hakika ya Tawassul hizo na hukmu yake kisheria.
Makala hii itaweka wazi kila jambo linalohusiana na Tawassul, nini maana ya Tawassul kilugha, nini maana ya Tawassul kisheria (kidini) ni aina gani ya Tawassul zilizokubaliwa kwa mujibu wa mafunzo ya Qur’aan na Sunnah sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)na ni Tawassul gani zisizofaa na kwa nini? Hoja zinazotegemewa na watetezi wa Tawassul zisizofaa na majawabu yake. Lengo la makala hii ni kumuelimisha Muislamu mambo yaliyofichwa muda mrefu na walimu wetu ima ni kwa uchache wa elimu au kwa sababu ya maslaha yao ya kidunia.
Ewe ndugu yangu msomaji wa makala hii jitahidi kufuatilia mfululizo wa makala haya na InshaAllah utajikuta katika hali ya kujikomboa kidini na kiuchumi, na kutokubali kuchezewa tena. Nakutakia usomaji mwema na wenye manufaa.

Itaendelea...